Azam 3-2 Coastal Union | Highlights | NBC Premier League 27/11/2022



Ilikuwa ni mechi ya tamu, mechi ya magoli matano… Idd Seleman Nado akifunga goli dakika ya 90+9 na kuipa ushindi Azam FC dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Coastal walitangulia kwa goli la Maabad Maulid dakika ya 13 kabla ya James Akaminko kuisawazishia Azam dakika ya 56 lakini Hamadi Majimengi alifunga bonge la goli dakika ya 85 na kufanya mambo yawe 2-2.

Baada ya hapo, Idd Seleman akapeleka msiba Tanga….

Tazama mambo yalivyokuwa…

Camiseta Manchester United 2ª Equipación 2019/2020 Comparez et achetez des Maillots de football enfant pas cher avec. Retrouvez les dernières tendances mode pour filles, garçons et bébés.

36 comentarios

  1. Kipa wenu dakika nne za mwanzo ziloengezwa kalala sasa mulitaka aumalize mpira wakati dakika hazikuchezwa nyie vip ss ndio tushashinda na tutaendelea kushinda tukutane kituo kinachofata

  2. Watu wengi wanalalamika kuhusu muda, hivi mnaanzaje kumlaumu refa wakati anasimamsha muda kwa kila tukio linazuia kuendelea kwa kabumbu? Mulitaka hata wachezaj wa Coastal wanapolala tuseme kuwa kabumbu linaendelea????
    This is a football we have to be serious

  3. Majitu yanacholalamika ata akionekani n ushabiki tu kuhofia nafasi yapili Mana hakuna gol la offside na hakuna makosa mengi lkn swala la muda kila tmu c jukum lake kuutumia ipasavyo

  4. Azam tafuteni wachezaji wa kucheza mpira wa kushindana siyo kinyume chake, mara nyingi Azam wanapata magoli wapinzani wanarudisha mfululizo, ushindi unakuwa kama ngekewa tu. Huyo golikipa silolote si chochote mmeramba garasa, la sivyo kila mwaka mtawaachia Simba na yanga kubeba vikombe nyinyi mmpo hapohapo.

Los comentarios están cerrados.